Bwawa la Kidunda lakutanisha taasisi sita, kujadili utekelezaji wake

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:52 PM Oct 10 2025
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri.
Picha:Mpigapicha Wetu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri.

Viongozi kutoka taasisi sita ikiwemo wizara, wamekutana kujadili njia za pamoja katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa bwawa la Maji Kidunda.

Lengo la kikao hicho ambacho kimefanyikia mkoani Morogoro ni kuhakikisha mradi huo mkubwa na wa kihistoria unakamilika kwa wakati. 

Wizara hizo ni, Wizara ya Maji, Wizara ya Mifugo na Uvivu, Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati. Pia, Tume ya Mipango na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wameshiriki.  

Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 329 ambao utanufaisha mikoa ya Dar ss Salaam, Pwani na Morogoro katika huduma za upatikanaji majisafi na yenye uhakika. 

Akiongoza kikao kazi hicho, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amesema ushirikiano wa kisekta utasaidia  utekelezaji wake ambao unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 utafanikis 

"Tumekutana Wizara muhimu za kisekta zinazochangia ukamilishaji wa mradi wa Kidunda ili kubaini maendeleo ya mradi sambamba na kukwamua changamoto zilizopo ili mradi ukamilike kwa wakati. 

Ushirikiano wa kisekta ni muhimu sana kwani kwa pamoja tutasaidiana kutatua changamoto na kuja na mipango bora zaidi ya utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa wananchi" amesema Mhandisi Mwajuma. 

Mhandisi Mwajuma amesem katika kipindi cha utekelezaji wa mradi ni muhimu kushirikiana kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na ulinzi wa vyanzo vya maji ili pindi bwawa litakapokamilika kusiwepo na changamoto za uharibifu wa mazingira na kupelekea bwawa kutojaa inavyohitajika. 

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Dkt Musa Ali Musa ametoa maelezo kwa watekelezaji wa mradi wa bwawa la Kidunda kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wananchi wanaozunguka mradi huu ili kuepuka malalamiko yanayoweza kuleta dosari katika mradi.