Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amewatoa hofu Watanzania kwamba, wasiogope kwenda kupiga kura Oktoba 29, 2025, kwamba yeye ni Amiri Jeshi Mkuu wa nchi na kibati kikipasuka wako nao.
Dk. Samia ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Bariadi, mkoani Simiyu.
”Niseme niwatoe hofu kuna watu wanatishatisha kufanya watu wasitoke Oktoba 29, 2025.
“Ninataka kuwaambia ninayezungumza hapa ni Amri Jeshi Mkuu wa nchi hii. Ninataka kuwaambia wasidhubutu, kibati kikipasuka sisi tuko nao tumejipanga vizuri tokeni kapigeni kura rudini nyumbani mkapumzike. Hakuna mtu wa kuwapa hofu mkapige kura,” ameahidi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED