JK: Wanaoniombea mabaya watatangulia wao

By Gwamaka Alipipi , Nipashe
Published at 05:12 PM Oct 10 2025
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete
Picha: Mpigapicha Wetu
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amewajibu watu wanaomzushia kifo akisema yeye ni mzima wa afya wala haumwi na kichomi, kwamba wanaomwombea mabaya watatangulia wao.

Ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Kikwete amesema: "Kuna watu wananizushia mara nimekufa, wengine wanasema ninaumwa. Mimi ni mzima wa afya, afya yangu ni nzuri, sina ninapougua, wataugua wao na nitashiriki mazishi yao"