Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitisha kikao maalum kwa wanachama waliowania ubunge mwaka 2020 na wale wanaopanga kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa watia nia wa Kanda ya Kati, Dodoma na Katibu wa CHADEMA Kanda hiyo, Ashura Masoud, kikao hicho kitafanyika Aprili 3 katika Ofisi Kuu za chama, Mikocheni, Dar es Salaam, kuanzia saa nne asubuhi.
Hatua hiyo inakuja wakati ambapo chama hicho kinaendelea na msimamo wake wa ‘no reforms, no election,’ hali inayozua mjadala kuhusu ushiriki wake katika uchaguzi ujao.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Dodoma, Aisha Madoga, amefafanua kuwa kikao hicho si cha watia nia wa mkoa huo pekee, bali kinawahusu wanachama wote wa chama hicho wenye nia ya kugombea ubunge nchi nzima.
Kikao hicho kinaweza kutoa mwanga juu ya mwelekeo wa CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED