Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kimekiri kupokea taarifa ya kujiuzuru kwa aliyekuwa mwanachama wake, Eugene Kabendera, kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.
Akizungumza kwa niaba ya chama, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Uenezi, Ipyana Samson, amesema chama kinatambua mchango mkubwa alioutoa Kabendera katika kipindi alichokuwa ndani ya chama hicho.
“Tumeona barua yake ambayo imesambaa mitandaoni, tunamtakia kila la heri huko aendako. CHAUMMA sasa kinaelekeza nguvu zake zote kwenye maandalizi ya tukio kubwa la uzinduzi wa Oparesheni CHAUMMA for Change (C4C), linalotarajiwa kufanyika Mwanza, Juni 1, 2025,” amesema Samson.
Kabendera alikuwa miongoni mwa wanachama waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho na kuchangia katika kukijenga.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED