Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimeahirisha Mkutano wake Mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 28 na 29 Mei mwaka huu, jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa CWT, Mkutano huo sasa umepangwa kufanyika tarehe 8 na 9 Juni mwaka huu, katika mkoa huo huo wa Dodoma.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa sababu kuu ya kusogeza mbele Mkutano huo ni kupisha Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 na 30 Mei katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma.
Akizungumzia hatua hiyo, Katibu wa Wabunge wa CCM Bungeni,Rashid Shangazi, amelipongeza Chama cha Walimu Tanzania kwa uamuzi huo wa kizalendo.
Amesema kuwa hatua hiyo inaonesha ukomavu wa kiuongozi ndani ya CWT, pamoja na kuonyesha nidhamu na heshima kwa taasisi za kitaifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED