Dk. Mwinyi aahidi ujenzi wa gati Kisiwa cha Kojani kuboresha huduma za afya

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 04:14 PM Oct 07 2025
Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali itaangalia uwezekano wa kujenga gati au kuchimba sehemu maalum ya bandari katika Kisiwa cha Kojani, ili kurahisisha huduma za usafiri wa boti ya wagonjwa kufanya kazi masaa 24 bila vikwazo.

Dk. Mwinyi alitoa ahadi hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kisiwa hicho, mara baada ya kukabidhi boti ya kubeba wagonjwa, iliyotolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa Kojani na maeneo jirani.