Dk. Nchimbi atua Sumbawanga, kufanya mikutano miwili leo

By Gwamaka Alipipi , Nipashe
Published at 01:36 PM Sep 08 2025
Mgombea mwenza wa urais CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi
Picha: CCM
Mgombea mwenza wa urais CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

Mgombea mwenza wa urais CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ajili ya kuendelea na kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Balozi Dk. Nchimbi amewasili leo Septemba 8 wilayani Sumbawanga akitokea mkoani Kagera, na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Sumbawanga.

Leo, Balozi Dk. Nchimbi atafanya mkutano mdogo katika viwanja vya Lahela na baadaye mkutano mkubwa Kalambo.