Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, kesho Septemba 6 anatarajiwa kurejesha fomu yake ya uteuzi katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ZEC, Dk. Mwinyi atakuwa mgombea wa kwanza kurejesha fomu hiyo kati ya wagombea wote 17 waliochukua fomu tangu zoezi hilo lianze Agosti 28 mwaka huu.
Dk. Mwinyi, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar, alichukua fomu ya kugombea urais Agosti 30 kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa ZEC, zoezi la urejeshaji wa fomu litafungwa Septemba 10, huku kampeni zikitarajiwa kuanza Septemba 11, 2025.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED