Wizara ya Elimu Zanzibar yaja juu video wanafunzi wakicheza muziki

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 02:34 PM Sep 05 2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Khamis Abdulla Said.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imekemea vikali maudhui ya video zinazojirudia kusambaa mitandaoni zinazowaonesha wanafunzi wa shule ya msingi wakicheza muziki kinyume na maadili.

Video hizo zinaonyesha wanafunzi wakicheza wakiwa kando ya gari lililokuwa likibeba wafuasi wa chama fulani cha siasa visiwani Zanzibar, ambao walikuwa wakiwasindikiza wagombea kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi majimboni, kuhusiana na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.