Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amewataka wanachama wa CCM kuimarisha mshikamano na kurejesha umoja wao ili kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Faris alitoa wito huo Septemba 4, 2025, wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi jimbo la Missenyi uliofanyika katika kata ya Bwanjai.
Amesema kipindi cha kampeni ni cha kuhubiri mshikamano na mshikikano wa wanachama, badala ya kutumbukia kwenye maneno ya mipasho na malumbano ambayo yanaweza kuhatarisha ushindi wa chama hicho katika maeneo mbalimbali.
“Huu ni wakati wa mshikamano na mshikikano, sio kipindi cha kutambiana au kupeana maneno ya mipasho. Tukifanya hivyo tutakuwa tunahatarisha ushindi wa chama chetu,” alisema Faris.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED