Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kwamba mojawapo ya ahadi za chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ni ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua madini.
Ametoa ahadi hiyo leo, Agosti 4, mkoani Shinyanga, wakati akizungumza na wananchi katika mwendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Dk. Nchimbi amesema CCM inatambua umuhimu wa madini mkoani Shinyanga, hivyo ujenzi wa kiwanda hicho utasaidia kuongeza thamani ya madini yanayopatikana mkoani humo. Aidha, alisema chama hicho kitalenga kuboresha mazingira ya uwekezaji ili malighafi zitengenezwe hapa nchini na hivyo kukuza pato la taifa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED