Machifu wachafukwa wanaombeza Samia mtandaoni

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 03:36 PM Sep 04 2025
Machifu wa mila wachefukwa wanaomtukana Samia mtandaoni
Picha: CCM
Machifu wa mila wachefukwa wanaomtukana Samia mtandaoni

Machifu wachafukwa na kitendo cha baadhi ya watu wanaomtukana Rais Samia Suluhu Hassan, katika mitandao ya kijamii na kuamua kumpa ulinzi, kama wasaidizi wake.

Kadhalika wamehoji kwa nini wanaaohusika na mitandao wanashindwa kudhibiti matukio ya aina hiyo.

Mwenyekiti wa Machifu Mbeya Vijijini, Chifu Soja Masoko, akizungumza katika mkutano wa kampeni ya mgombea urais CCM leo Septemba 4, 2025, unaoendelea Mbalizi, mkoani Mbeya, wametoa msimamo wao juu ya matukio hayo.

Chifu Masoko amesema wao wako machifu zaidi 270, wakiwaeleza wanaofikiri wanawake hawawezi kufanya kazi kwa sasa wanaona aibu.

“Tuna hasira, wewe ni Chifu Hangaya, Machifu wote Tanzania ni wasaidizi wako, tunapoona kuna baadhi ya watu wanabeza unayofanya na wanadiriki kukutukana katika mitandao ya kijamii hatupendezwi kuona picha mbalimbami kwenye mitandao, wakati tunasikia kuna namna ya kudhibiti.

“Anayeleta vitu vya ajabu ni kwa nini watu wa mitandao wanaruhusu  watu wa ajabu kusababisha hali ya hewa kuchafuka katika nchi yetu. Hatupendezwi Machifu wa Tanzania nzima hata kama hawako hapa,amesema.

Chifu Masoko amesema wanaofanya hivyo wanawasukuma Machifu watumie mambo yao ya kimila, akisisitiza mtu wa namna hiyo akemewe.

Amesema katika nchi hii hawajawahi kupata mtikisiko na  kuhoji anayetaka kuwaletea hilo ni nani.

Kutokana na hayo yanayoendelea, Chifu Masoko amesema wamemwandalia zawadi ambayo ni fimbo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Samia popote atakapokuwa anakwenda awe salama kuwa yuko mikononi mwa wazee.

Kadhalika wamempatia mgolole mweupe ukilenga uchaguzi mwezi Oktoba mwaka huu ufanyike kwa amani na kiti chenye miguu mitatu, ambacho huzikiwa machifu, ambapo ameelezea kuwa wakimtunuku mtu kiti hicho akae, hakuna kuyumba wala kuyumbizwa.

Wazee wa mila pia wamempatia zawadi ya mbuzi ili akale akiwa njiani.