Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amewataka wagombea wote wa chama hicho—wale waliopata nafasi na hata ambao hawakufanikiwa kupenya katika mchujo wa Uchaguzi Mkuu—kuvunja makundi na kuungana ili kukiimarisha chama kuelekea kwenye uchaguzi.
Samia ametoa wito huo leo Septemba 5, 2025, wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Njombe.
“Niungane na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Deo Sanga, ambaye amezungumzia suala la kuvunja makundi. Nimpongeze kwa jambo hili. Niombe sana wagombea wote waliofanikiwa na ambao hawakufanikiwa, tuvunje makundi, turudi kuwa chama kimoja ili tuingie kwenye uchaguzi tukiwa na nguvu kubwa,” amesema Samia.
Amewasisitiza wanachama na viongozi wa CCM kuendeleza mshikamano, mshikikano na mshirikiano, akisema mshindi wa kweli ni chama chao kikibaki imara na kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED