Othman Masoud awasilisha Hati ya Kiapo kugombea urais Zanzibar

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 08:54 PM Sep 08 2025
Othman Masoud awasilisha Hati ya Kiapo kugombea urais Zanzibar
Picha:Mpigapicha Wetu
Othman Masoud awasilisha Hati ya Kiapo kugombea urais Zanzibar

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Othman Masoud Othman, leo Septemba 8, 2025, amewasilisha Hati ya Kiapo mbele ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Hati hizo, ambazo ni sehemu ya mchakato wa uteuzi wa kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar, zimepokelewa na kuapishwa katika Mahakama Kuu iliyopo Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja, na Jaji Said Hassan Said.

Shughuli hiyo pia ilishuhudiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhan Abdallah.