Hatma kesi ya Mpina kufahamika Septemba 11

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 07:39 PM Sep 08 2025
Hatma kesi ya Mpina kufahamika Septemba 11
Picha: Mpigapicha Wetu
Hatma kesi ya Mpina kufahamika Septemba 11

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, inatarajiwa kutoa hukumu ya shauri namba 21692 la mwaka 2025 lililofunguliwa na Bodi ya Wadhamni ya Chama cha ACT-Wazalendo na ndugu Luhaga Joelson Mpina dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 11, 2025.

Shauri hilo lipo mbele ya Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji wa Mahakama hiyo Jaji Abdi Kagomba, ambalo linahusu kurudishwa kwa mgombea wa  kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT- Wazalendo kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea. 

Kutokana na kukamilika kwa uwasilishwaji wa hoja kwa njia ya maandishi kwa pande zote mbili shauri hilo leo limeanza kusikilizwa kwa ajili ya uwasilishwaji wa ana kwa ana ili kutoa nafasi kwa pande zote kufafanua hoja zao ikiwamo kujibu maswali kutoka kwa majaji wa jopo hilo. 

Baada ya pande zote mbili jana kumaliza kuwasilisha hoja zao mbele ya jopo la majaji hao, Jaji kiongozi wa jopo hilo Jaji Kagomba, amesema wamemaliza kusikiliza hoja za pande zote mbili hivyo hukumu ya shauri hilo itatolewa Septemba 11, 2025.