Salum Mwalimu: Uchaguzi usichukuliwe kwa mazoea wala kishabiki

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 08:35 PM Sep 08 2025
Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu.

Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amewataka Watanzania kutochukulia uchaguzi kwa mazoea au kishabiki, bali kufanya maamuzi yenye kuzingatia maslahi ya maendeleo ya Taifa.

Akihutubia wakazi wa Mji wa Magugu, mkoani Manyara, Mwalimu alisema bado wapo wananchi wanaoingia kwenye uchaguzi kwa misingi ya ushabiki wa vyama, bila kuangalia uwezo na mipango ya wagombea.

Alisisitiza kuwa kura ya mwananchi inapaswa kuwa mkataba kati yake na kiongozi anayemchagua, ili kuhakikisha anapata huduma bora na muhimu.

“Unapokwenda kupiga kura, unamchagua kiongozi kwa sababu umemuamini atakuboreshea huduma, si kwa sababu ya chama chake,” alisema Mwalimu.