KIONGOZI wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu amesimulia shuruba walizopata viongozi wa upinzani nchini Angola ikiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais, Othaman Masoud kusimama kwa saa nane bila kupokelewa wala kupewa mahali pa kukaa.
Akizungumza katika mahojiano maalum na chombo kimojawapo cha habari nchini, Kiongozi huyo amesema mpaka sasa hawajajua walipokosea kwa kuwa walifuata taratibu zote za kuingia nchini humo na kuwasiliana na wenyeji wao.
“Makamu wa Kwanza wa Rais (Othman Masoud ) yeye alikaa pale uwanja wa ndege zaidi ya masaa 8 bila kupokelewa wala kukaa sehemu yoyote, masaa mawili tuliyokuwa tumefika pale tulikuwa tumesimama tu na tuliwaomba watupatie hata sehemu ya kukaa wakati wanatueleza hayo masuala lakini hawakutusikiliza” alisema Dorothy
“Tulikuwa na mawasiliano mazuri na wenyeji wetu, tulifanya maandalizi yote na kufuata taratibu zote zilizotakiwa”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED