Katele arudisha fomu ya udiwani, ahadi kutatua changamoto ya maji Pangani

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 05:24 PM Aug 27 2025
Katele arudisha fomu ya udiwani, ahadi kutatua changamoto ya maji Pangani
Picha: Mpigapicha Wetu
Katele arudisha fomu ya udiwani, ahadi kutatua changamoto ya maji Pangani

Mgombea wa nafasi ya udiwani Kata ya Pangani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Katele, amerejesha fomu ya kugombea nafasi hiyo huku akiahidi kushughulikia kero ya muda mrefu ya maji katika kata hiyo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fomu, Katele amesema suala la maji ni moja ya vipaumbele vyake vya msingi, na atashirikiana na serikalini kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi wa haraka.

“Wizara tayari imeanza utekelezaji wa mradi wa maji, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa na utulivu wakati changamoto hii inaendelea kushughulikiwa,” amesema.

Mgombea huyo pia amebainisha kuwa kipaumbele kingine ni kuimarisha mazingira ya kiuchumi ili wananchi waweze kunufaika na kupunguza umasikini.

Madiwani wote wa CCM katika kata hiyo pia wamefanikiwa kurejesha fomu zao, kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya udiwani.