Zanzibar : Vyama 17 vyaweka ratiba ya uchukuaji fomu za urais

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 04:53 PM Aug 28 2025
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC, Thabit Idarous Faina.
Picha: Mtandao
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC, Thabit Idarous Faina.

Vyama 17 vya siasa tayari vimeshawasilisha barua za ratiba ya uchukuaji wa fomu kwa wagombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar, kufuatia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) leo kufungua rasmi milango ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC, Thabit Idarous Faina, amesema mgombea wa CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ndiye atakayekuwa wa kwanza kuchukua fomu hiyo Agosti 30, mwaka huu, saa 4:00 asubuhi.

Baada ya Mwinyi, ratiba ya siku hiyo itaendelea kama ifuatavyo:

  • Saa 5:00 asubuhi, mgombea wa NLD atachukua fomu.

Saa 6:00 mchana, mgombea wa AAFP.

  • Saa 7:00 mchana, mgombea wa CUF.

Saa 8:00 mchana, mgombea wa TLP.

  • Saa 9:00 mchana, mgombea wa NRA.

Faina ameongeza kuwa kwa tarehe 31 Agosti, vyama vitatu vitafanya zoezi hilo ambapo:

  • Saa 3:00 asubuhi, mgombea wa NCCR Mageuzi atachukua fomu.

Saa 4:00 asubuhi, mgombea wa ACT Wazalendo.

  • Saa 5:00 asubuhi, mgombea wa CCK.

Kwa siku ya Septemba 1, wagombea wa vyama vya DP na Makini wanatarajiwa kuchukua fomu zao, huku ZEC ikieleza kuwa tayari vyama vyote vimeshapewa maelekezo kuhusu taratibu za uchukuaji wa fomu.