Uzinduzi wa kampeni CCM kicheko kwa wajasiriamali

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 03:49 PM Aug 28 2025
Uzinduzi wa kampeni CCM

Uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaoendelea katika viwanja vya Tanganyika Parkers, Dar es Salaam, umeleta kicheko kwa wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na uuzaji wa vyakula na vimiminika, wakieleza namna walivyotumia fursa ya mkutano huo kujiingizia kipato.

Rehema Juma, mkazi wa Kawe, anasema aliposikia kuna mkutano huo aliamua kununua maji ya jumla ambayo anayauza rejareja viwanjani huko.

“Ninauza na ninaokota chupa zilizotumika ambayo nayo ni sehemu ya kujiongezea kipato,” anasema.

Asha Abdallah, mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, anasema amefika uwanjani hapo tangu asubuhi ili kuuza maandazi.

“Ninamshukuru Mungu si haba nimepata nimeongeza kitu kuliko ningekaa nyumbani,”  anasema.