"CHAUMMA tutajenga viwanda vya kubangua korosho zaidi ya 20. Sera yetu haiishii tu kwenye kuchochea viwanda, itahakikisha mkulima mmoja anapata mashine ndogondogo zenye teknolojia rahisi ili kila mkulima abangue mweyewe na kuziua zikiwa zimebanguliwa na kunufaisha.
"Kwa hiyo CHAUMMA itapiga hatua moja mbele kunyanyua kilimo na kuipandisha thamani ya korosho, tukifanya hivi tutainua kipato na kuboresha maisha ya wananchi." Amesema Mkurugenzi wa itikadi, Mafunzo na Oganizesheni.
Amesema asilimia 90 ya korosho inayouzwa haijabanguliwa.
"Na ikiuzwa hivyo bila kiwango, haina faida kwa wakulima, kwa hiyo kama kungekuwa na viwanda vya kutosha vya kubangua Korosho, wakulima wote wangeuza korosho ikiwa imebanguliwa"
"Kilo moja ya Korosho iliyobanguliwa ni zaidi ya sh.10,000 na isiyobanguliwa ni sh.4000 katika kila kilo akiuza isiyobanguliwa anapoteza zaidi ya sh.6000."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED