Kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Pwani, Boniphace Jacob, pamoja na Afisa wa masuala ya Haki za Binadamu, Godlisten Malisa imetajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Washatakiwa hao wanatetea kupitia wakili wao, Dickson Matata, huku kesi hiyo ikiwa katika hatua ya usikilizwaji wa mashahidi.
Awali, mawakili wa Jamhuri waliwasilisha ombi la mashahidi kusikilizwa kwa siri, lakini mahakama ililikataa. Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulikata rufaa Mahakama Kuu, na uamuzi wa rufaa hiyo bado unasubiriwa.
Kesi imepangwa kutajwa tena tarehe 4 Septemba mwaka huu saa 5:00 asubuhi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED