Watendaji wa uchaguzi waapishwa, waanza mafunzo maalum Njombe

By Elizabeth John , Nipashe
Published at 06:32 PM Jul 16 2025
Watendaji wa uchaguzi waapishwa, waanza mafunzo maalum Njombe
Picha: Mpigapicha Wetu
Watendaji wa uchaguzi waapishwa, waanza mafunzo maalum Njombe

Watendaji wa Uchaguzi wa ngazi ya Jimbo kutoka mikoa ya Njombe, Ruvuma na Iringa wameapishwa Julai 15 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Liad Chamshana.

Kiapo hicho kinawahusu kujitoa uanachama wa chama chochote cha siasa pamoja na kutunza siri, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi.

Tukio hilo limefanyika katika Kituo cha Njombe Mjini, ambapo mafunzo maalum yanayoandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yanaendelea kuanzia tarehe 15 hadi 17 Julai 2025.

Mafunzo hayo yanalenga kuwaandaa Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi pamoja na Maafisa Ununuzi kwa ajili ya uchaguzi ujao.