“Kwenye boma la watu wengi hawakosekani vichaa, tuachie tuwafundishe adabu”

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 08:57 PM Jun 18 2025
Naibu Katibu Mkuu Chamaa Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Mongella
Picha: Mtandao
Naibu Katibu Mkuu Chamaa Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Mongella

Naibu Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Mongella, amesema katika boma la watu wengi akitolea mfano Kanda ya Ziwa ambayo ameitaja ni moja ya ngome ya CCM, hawakosekani vichaa.

Hivyo, Mongella amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan awaachie watu wa namna hiyo watatokea vijana na wana-CCM kuwafundisha adamu.

Mongella ametoa kauli hiyo leo Juni 18, 2025, katika mkutano wa hadhara wa majumuisho Bariadi, Simiyu, katika ziara ya Rais Samia.

Amewataka wana Simiyu na Watanzania wasibweteke, kwani adui bado yuko.

“Mheshimiwa Rais nakumbuka nilipokuwa mdogo, pale kwenye boma letu tulikuwa wengi, lakini nakumbuka kuna bwana mmoja alikuwa na akili siyo nzuri sana na kwa sababu kwenye boma tulikuwa wengi, alikuwa kila siku anakula nyumbani.

“Lakini siku moja akamwambia bibi, wewe siku moja nitakuua, kwa hiyo ikabidi wana boma pale vijana wamtulize kidogo kwa kumchapa viboko,” anasimulia.

Mongella anasema kwenye boma la watu wengi, kama ilivyo kwenye kanda hiyo, hakuwezi kukosekana vichaa mmoja au wawili.

“Ninakuomba utuachie hawa watatokea vijana na wanaCCM kuwafundisha adamu,” amesema Mongella huku akimwakikishia Rais Samia kuwa Kanda ya Ziwa ni salama kwa chama hicho kutokana na mwitikio mkubwa ambao ameupata katika ziara hiyo.