Mgombea mwenza wa urais CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi amewasili mkoani Mwanza leo Agosti, 29 tayari kwa kuanza ziara ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu.
Dk. Nchimbi akiwasiri katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza majira ya saa 2 asubuhi na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi ( INEC) Dk. Nchimbi leo atafanya mkutano mdogo Kwimba na baadaye mkutano mkubwa Ilemela na Nyamagama.
Akizungumza baada ya kuwasili mkoani Mwanza, Dk. Nchimbi amesema: "Tupo tayari na timamu kuanza kampeni za kuipeperusha bendera ya chama.
Amesema pia, timu yake ipo tayari kuitangaza na kuitekeleza Ilani ya CCM.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED