Mgombea udiwani wa Viti Maalum Tarafa ya Emboreet, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, Rehema Naaman (CCM), amefariki dunia ghafla baada ya kudaiwa kuugua homa ya mapafu.
Mgombea huyo wa udiwani, alipoteza maisha Septemba 20 mwaka huu, akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Kwa mujibu wa Katibu wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Simanjiro, Tichomo Sangija, marehemu Rehema Naaman, alishiriki kampeni za chama hicho za mwanzoni na baadae aliugua ghafla na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Amesema wakati wa uhai wake, Rehema pia alikuwa Mwenyekiti wa UWT, Kata ya Loiborsiret.
"UWT inawapa pole wale wote waliofikwa na msiba huu Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe," amesema Sangija.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED