Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameungana na viongozi wa chama, viongozi wa dini pamoja na wananchi katika hafla ya kuuaga mwili wa Hawa Moses Kulola, mwanachama wa chama hicho aliyeaga dunia jana baada ya kuanguka ghafla kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Kijini, mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungumza katika tukio hilo, Othman amesema ameguswa sana na msiba huo mkubwa, akiwasihi ndugu wa marehemu kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
“Marehemu alikuwa mstari wa mbele muda wote katika kupigania haki na demokrasia, akibeba sauti ya wananchi na kupinga dhulma,” amesema Othman.
Aidha, amesisitiza kuwa njia pekee ya kumuenzi marehemu ni kuendeleza mapambano ya kudai mabadiliko na demokrasia ya kweli Zanzibar.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED