Serikali kuongeza ajira Sekta ya Afya na Utalii – Dk. Mwinyi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:36 PM Sep 22 2025
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa serikali yake itaendelea kuongeza nafasi za ajira hasa katika sekta ya afya na utalii, ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira na kuboresha huduma kwa wananchi.

Akizungumza katika moja ya mikutano ya kampeni, Dk. Mwinyi amebainisha kuwa ajira mpya zitajikita zaidi kwa wauguzi na wataalamu wa afya ili kuhakikisha huduma bora za afya zinafika hadi vijijini. Alisema serikali inaendelea kufanyia kazi upungufu wa watumishi katika sekta hiyo na itaweka kipaumbele kwa wahitimu wa fani mbalimbali za afya.