MWANDISHI wa habari gazeti la Nipashe na Nipashe Digital, Halfan Chusi ameibuka mteule katika Tuzo za Zanzibar Communication Excellence Award (ZCEA).
Katika tuzo hizo, Chusi anawania kipengele cha Mwandishi Bora wa Habari katika Mitandao ya Kijamii.
Utoaji wa tuzo hizo, unatarajiwa kufanyika kesho kuanzia majira ya jioni, Unguja, Zanzibar.
Mapema April, mwaka huu, Msajili wa Hazina Zanzibar, Waheed Muhamed Ibrahim Sanya, katika mkutano na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Tuzo za Umahiri wa Mawasiliano kwa mara ya kwaza Zanzbar;
Alisema vyombo vya habari nchini ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo ya jamii na kuwapo uwajibikaji kwa uwazi wa shughuli zinazofanywa na serikali na mashirika ya umma katika ngazi za taifa.
Ameyasema amefurahishwa sana kuona kuwa Zanzibar imezinduliwa Tuzo za Umahiri katika Mawasiliano ya Umma (Zanzibar Communication Excelence Award), ambazo zinalengo kutambua na kuhamasisha wadau wa habari wakiwamo waandishi wa habari na mawasiliano wa serikali ns mashirika ya umma.
Alieleza ofisi yake kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, wana matumaini makubwa kuwa tunzo hizo zitaleta mapinduzi makubwa kwa maendeleo ya Zanzibar kupitia uchocheaji na utoaji wa taarifa sahihi na zenye weledi kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Mkururugenzi ya wa Institute of Public Reletion Tanzania (IPRT) Dk. Titus Solomon, amesema tasisi yake tayari imeaza kutoa mafunzo hayo katika ngazi mbalimbali ya Jeshi la Polisi, ZRA, Chama cha walimu, Shirikisho la vyama vya ushirika na taasisi nyengine hapa nchini.
Mratibu wa tuzo hizo, Lufunyo Mlyuka, amesema kuwa kuanzia Julai mwaka huu, wanatarajia kutoa tuzo hizo zilizoshindanishwa na wataaza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kabla ya kutoa tuzo hiyo.
Ofisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Mwantanga Juma Khamis, akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo, Salum Ramadhan, aliwataka wandishi wa Habari kuichangamkia fursa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED