Serikali yamzawadia gari Mkuu wa Nsumba Sekondari

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 05:34 PM Aug 06 2025
Serikali yamzawadia gari Mkuu wa Nsumba Sekondari.
Picha: Mpigapicha Wetu
Serikali yamzawadia gari Mkuu wa Nsumba Sekondari.

Halmashauri ya Jiji la Mwanza, mkoani hapa imemzawadia Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Nsumba, Denis Mwakisimba kwa utendajikazi mzuri ulioifanya shule hiyo kuendelea kufanya viziri kwa mfululizo.

Kadhalika walimu wa Shule hiyo wameahidiwa kupatiwa zaidi ya Sh.milioni 18 ambazo watagawana kwaajili ya motisha ya kuendelea kuweka bidi katika ufundishaji.

Akizungumza leo Agosti 6, 2025 mara baada ya kukabidhi gari hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amewataka walimu wote kuendelea kufanya vizuri bila kujali nafasi wala vyeo walivyo navyo.

“Nimeambiwa Mkuu huyu wa Shule hajaanza hapa tu kila alipopelekwa alijitahidi kuhakikisha anafanya mabadiliko na kuinua shule husika, haiwezekani mtu unakaa sehemu hata mchango wako hauonekani tafuteni sehemu ambayo mnaweza zaidi wekeni alama,”amesema.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba amesema licha ya Mkoa kutoa motisha kwa shule, walimu na wanafunzi, kama Halmashauri wamepanga kuendelea kuwapa motisha hasa wale watakaosaidia kuinua ufaulu hasa katika elimu msingi.

Mkuu huyo wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Nsumba alisema ataendelea kushirikiana na walimu wengine pamoja na uongozi wa serikali ya Halmashauri na Mkoa kuhakikisha wanafikisha kiwango chaelimu juu zaidi.

Kabla ya zawadi hiyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza iliandaa tuzo pamoja na zawadi mbalimbambali kwaajili ya shule, walemu na wanafu waliofanya vizuri na kuinua Mkoa katika ufaulu.

Zawandi hizo zimetolewa katika vipengele mbalimbali ambako kwa kila kipengele mshindi wa kwanza alizadiwa Sh.600,000 wa pili 500,000 na watatu 400,000 lengo likiwa ni kuongeza motisha kwa walimu na wanafunzi.

1