Mabingwa JKCI, Marekani watibu umeme wa moyo wagonjwa 10

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 04:18 PM Aug 06 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya wa JKCI na
wenzao kutoka Shirika la Madaktari Africa la nchini Marekani
Picha: JKCI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya wa JKCI na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Africa la nchini Marekani

TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imeokoa maisha kwa wagonjwa 10 wenye matatizo ya mapigo ya moyo.

Huduma hiyo imetolewa kwenye kambi ya siku tano iliyofanywa na wataalamu wa JKCI, kwa kushirikiana na wenzao kutoka shirika la Madaktari Africa la Marekani.

Wataalamu wa afya ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani kumfanyia mgonjwa upasuaji mdogo wa moyo mgonjwa ambaye ana tatizo la mapigo ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano iliyomalizika hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mfumo wa Umeme wa Moyo kutoka JKCI, Dk. Yona Gandye, amezungumza hayo leo, jijini Dar es Salaam.
Wataalam wa afya kutoka Shirika la Madaktari Africa la nchini Marekani wakisoma taarifa fupi ya mgonjwa kabla ya kumfanyia upasuaji mdogo wa moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Zaidi ya wagonjwa 10 wenye matatizo ya mapigo ya moyo wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo
Amesema wagonjwa waliopatiwa matibabu ni wenye matatizo katika mfumo wa utengenezaji wa mapigo ya moyo na kusababisha moyo kwenda kasi kupita kawaida, kuzimia na kuwa katika hatari ya kupoteza maisha.