Ngoma bado ni nzito ndani ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kufuatia kuahirishwa mara kwa mara kwa muda wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu maamuzi muhimu yanayosubiriwa kwa hamu.
Tangu juzi, kumekuwa na mfululizo wa mabadiliko ya muda wa kutoa taarifa hizo. Awali, ilielezwa kuwa taarifa ingetolewa saa tano asubuhi, baadaye ikasogezwa hadi saa 11 jioni, kisha hadi saa 12 jioni. Hata hivyo, ilipofika saa 2 usiku, muda huo ukaahirishwa tena hadi saa 3:30 usiku.
Baada ya hapo, hakukuwa na taarifa yoyote hadi ilipokucha asubuhi ya leo, Julai 29, 2025, ambapo ilitangazwa kuwa majina yangetangazwa saa nne asubuhi. Hata hivyo, ilipokaribia saa nne, taarifa nyingine ikatolewa tena.
Kupitia ujumbe uliosambazwa kwa waandishi wa habari, ilielezwa hivi:
"Habari ya asubuhi wapiganaji, hongereni kwa majukumu. Mkutano wa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, utafanyika leo Julai 29, 2025, saa sita mchana. Mahali ni pale pale, ukumbi wa NEC, CCM Makao Makuu. Karibuni sana."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED