Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, John Mongela amewatahadharisha wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa kuwa wanafuatilia kwa karibu mienendo yao.
Akifungua mkutano huo leo jijini Dodoma, Mongela amesema: “Jana tulipata ajali mbili tatu, inawezekana leo ajali zikawa nyingi zaidi tusipokuwa waangalifu, hizi za kwenda kwenda chooni na wapi, tumekamata watu, ningeomba mwenyekiti kwa kikao chako cha leo siombii yatokee tuliyoyaona jana.”
Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, amewaasa wajumbe kutenda haki kwenye uchaguzi huo kwa kuwa wagombea wote ni sawa.
“Kama umetembelewa akili yako isiwe huko ulikotembelewa iwe katika kuchagua mtu unayemtaka wewe, fikra za fedha zisiwabadilishe, wapigieni kura watu ambao kila mmoja na akili yake na awe mtu atakayesaidia UWT,” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED