Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limepokea na kuchukua hatua baada ya taarifa kuhusu tukio la ukatili wa kijinsia kuenea kwenye mitandao ya kijamii, likihusisha Neema Nairot, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tukio hilo linadaiwa kuhusisha mchumba wa binti huyo pamoja na familia yake.
MajTarehe 26 Agosti 2025, Jeshi la Polisi limeanza ufuatiliaji wa kina kuhakikisha ukweli wa tukio unathibitishwa. Moja ya hatua zilizochukuliwa ni kumkamata Matunda Shambakubwa Longido (29), mfanyabiashara na mkazi wa Dakawa, Wilaya ya Mvomero, anayehusishwa na tukio hilo.
Aidha, binti aliyeathirika ameokolewa na kuhifadhiwa katika makazi salama ili kupewa ulinzi na msaada wa kisaikolojia.
Upelelezi unaendelea kwa ushirikiano na vyombo vingine vya haki jinai ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote waliohusika katika tukio hilo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED