Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameridhia msamaha wa faini zote kwa wananchi wenye madeni ya maji katika mamlaka mbalimbali nchini.
Aweso amesema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadilio ya Bajeti ya Wizara yake katika mwaka wa fedha 2025/2026.
“Katika hatua ya kugusa moja kwa moja maisha ya wananchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameridhia msamaha wa faini zote kwa wananchi wenye madeni ya maji katika Mamlaka mbalimbali.
“Mama Samia amesamehe fine hizo, hivyo wafike kwenye Mamlaka kwa ajili ya utaratibu wa kurejeshwa huduma ya maji hadi tarehe 31 Mei 2025.”amesema Aweso
Aidha, kwa wateja wote wenye madeni, Waziri Aweso amesisitiza kuwa ni fursa ya kipekee kwao kufika ofisi za Mamlaka za Maji kupewa utaratibu wa kulipa madeni hayo na kurejeshewa huduma mara moja bila usumbufu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED