Rais Dk. Samia kuhutubia Bunge leo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:50 AM Nov 14 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.
Picha: Mpigapicha Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa leo Novemba 14, 2025 kulihutubia bunge, ikiwa ni ishara ya kulizindua rasmi baada ya kukamilika kwa uteuzi wa viongozi wake wakuu, wakiwemo Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Naibu Spika.

Hotuba ya Rais Samia itakayoanza majira ya saa 9:00 alasiri, inatarajiwa kueleza vipaumbele vya serikali yake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, ikiwemo mikakati na ajenda za maendeleo, mwelekeo wa demokrasia na juhudi za kuimarisha umoja wa kitaifa.

Watanzania wanaisubiri hotuba hiyo ya kwanza ili kuweza kupata mwelekeo mpya katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Aidha, Dk. Samia anatarajia kumuapisha Waziri Mkuu mteule Dk. Mwigulu Lameck Nchemba asubuhi hii.