RAIS Samia Suluhu Hassan amewatakiwa kheri ya wanafunzi 595,816 wa kidato cha nne ambao wameanza mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari leo katika shule takribani 5,868 nchini.
Katika ujumbe alioutoa kupitia mitandao yake ya kijamii loe Rais Samia amesema idadi hiyo ya shule inatokana na nyongeza ya shule 305 mpya, ambazo ni mara yake ya kwanza kufanya mtihani wa kidato cha nne.
Amesema shule hizo ni matokeo ya kazi wanayoendelea kufanya kuhakikisha kila mtoto wa Tanzania ana uhakika wa kupata elimu bora.
“Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyewaongoza tangu elimu ya awali hadi leo awajalie utulivu mwifanye na kukamilisha vyema hatua hii muhimu kwenye maisha yenu.
“Ninawaombea pia mwendelee kuwa na nidhamu, upendo na bidii katika hatua zinazofuata kwenye maisha yenu. Serikali itaendelea kufanya kila inachoweza kuhakikisha ndoto zenu njema zinapata fursa na nafasi ya kukua na kustawi kwa manufaa yetu sote,” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED