Samia kujenga mabweni visiwani kuwaondolea adha wanafunzi

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 07:16 PM Oct 16 2025

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu Hassan.
Picha: CCM
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu Hassan.

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu Hassan, miongoni mwa ahadi zake katika sekta ya elimu ni kujenga mabweni kwenye visiwa ili kuwaondolea adha watoto wanaoishi huko, waweze kusoma bila changamoyo yoyote.

Ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 16, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Bukoba mjini, mkoani Kagera, ukihudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo Dk. Samia ameahidi kuongeza mabweni huku mengine yakijengwa katika visiwa vilivyoko mkoani humo ili kuondoa changamoto kwa wanafunzi na kuwafanya wasome vizuri.

Amesema watautunisha mfuko elimu ya juu ili vijana wapate fursa ya kupata elimu kupitia mikopo.