Samia, Nchimbi kuchukua fomu ya urais leo

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 11:35 AM Aug 09 2025
news
Picha Ibrahim Joseph
Msafara SaNchimbi wakienda kuchukua fomu.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeanza kuwasili katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo asubuhi, kumsindikiza Mgombea wa Urais kupitia chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia ataambatana na Mgombea Mwenza, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Wagombea hao wanatarajiwa kuchukua fomu saa tano asubuhi, huku shamrashamra kubwa zikiendelea nje ya Ofisi za INEC, zikiambatana na matarumbeta na nderemo kutoka kwa wafuasi wa CCM.

Mbali na CCM, vyama vingine vinavyotarajiwa kuchukua fomu leo ni Chama cha NRA na AAFP.