KAMATI ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), imetoa orodha ya mwisho ya majina ya wagombea 11 waliopenya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa shirikisho hilo, katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 16, mwaka huu mkoani Tanga.
Awali kulikuwa na majina 25, ambayo yalipelekwa kwenye kamati hiyo, lakini yalifyekwa katika hatua mbalimmbali na kubaki 19, labla ya mchujo mwingine ambako sasa yamebaki 11.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Kiomoni Kibamba, nafasi ya uenyekiti kuna jina moja tu la Wallace Karia, anayetetea kiti chake.
Nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji kanda namba moja ni Lameck Nyambaya na CPA Hosseah Hopaje, ndiyo waliopitishwa, kanda namba mbili yupo Khalid Abdallah Mohamed pekee, kanda namba tatu yupo James Patrick Mhagama, Evance Gerald Mgeusa na Cyprian Charles Kuyava.
Nafasi ya Ujumbe Kamati ya Utendaji namba nne jina lililopitishwa ni la Mohamed Omar Aden pekee, namba tano wapo wawili, Vedatus Kalwizira Lufano na Salum Kulunge, huku kanda namba sita sita, aliyepitishwa ni Issa Mrisho Bukuku.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED