Rais Samia Suluhu Hassan, amesema katika jitihada za kudhibiti visumbufu kwa mimea serikali imefanya jitihada mbalimbali ikiwamo kununua ndege maalum moja na ndege nyuki 101 kwa ajili ya kudhibiti na kuchunguza visumbufu vya mimea.
Samia, amesema hayo leo Agosti 8, 2025 jijini Dodoma, alipokuwa akifunga Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni.
“Pamoja na hayo serikali inaendelea kuimarisha upatinaji wa huduma za zana za kilimo kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya kilimo. Katika mwaka wa fedha 2024/2025 matrekta makubwa 500 na matreikta madogo 800 yalinunuliwa na tumeanzisha vituo jumuishi 45 vya kutoa huduma za zana za kilimo katika ngazi ya mkoa,”alisema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED