Rais Samia ataka maofisa ugani kuondolewa kwenye viyoyozi

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 06:14 PM Aug 08 2025

Rais Samia Suluhu Hassan
Picha: Ikulu
Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan, amemwagiza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dk. Ashatu Kijaji, kuwatoa maofisa ugani kwenye majengo ya maghorofa na viyoyozi ili kuwapeleka maeneo ambayo wakulima wataweza kuwafikia bila kuwapo na vikwazo.

Samia, amesema hayo leo Agosti 8, 2025 jijini Dodoma, alipokuwa akifunga Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni.

“Nataka kuwambia wewe pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwamba eneo hili la Nanenane sasa ni eneo linalokwenda kufanya kazi mwaka mzima huduma nyingi zitakuwa hapa maduka ya pembejeo,mbole na mambo ya ruzuku yatafanyika hapa.

“Kwahiyo niwaombe huduma za ugani zihamie pia hapa ili mwananchi akifika Nanenane awe anapata kila kitu ndani ya eneo moja kwahiyo ni waombe mjipange hivyo kwamba huduma za ugani pamoja na maeneo mengine ya nchi lakini hapa kuwe ni makao makuu ya huduma za ugani,”amesema