Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea Mwenza, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kesho wataenda Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuchukua fomu za kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo.
Makalla amesema kuwa baada ya kuchukua fomu, viongozi hao watakwenda Makao Makuu ya CCM kukutana na wanachama kwa ajili ya kusalimiana na kuzungumza.
Aidha, amesisitiza kuwa kutokana na kuwapo kwa ilani bora na wagombea wenye sifa, watanzania watawaelewa na kuwaunga mkono.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED