Mpina, Othman wapokelewa kwa kishindo unguja

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:25 PM Aug 09 2025
news
Picha Mpigapicha Wetu
Mpina, Othman wapokelewa kwa kishindo unguja

Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina, na mgombea mwenza Fatma Ferej, pamoja na mgombea wa urais wa Zanzibar Othman Masoud Othman wamepokelewa na maelfu ya wanachama wa chama hicho na wananchi wa Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha upande wa Unguja.

Mapokezi hayo yamefanyika leo Agosti 9, 2025 ikiwa ni muendelezo wa harakati za wanasiasa katika maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.