Vitendo vya ukatili wa kijinsia vyapungua

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 05:58 PM Aug 27 2025
Grafu kuhusu matukio hayo
Mchoro: Grace Mwakalinga
Grafu kuhusu matukio hayo

JITIHADA zinazofanywa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, zimeanza kuzaa matunda, baada ya takwimu mpya kuonesha kupungua kwa matukio ya ukatili nchini.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, matukio ya ubakaji yamepungua kutoka 8,185 mwaka 2023 hadi 7,670 mwaka 2024, sawa na upungufu wa asilimia 6.3. Vilevile, matukio ya ulawiti yameshuka kutoka 2,382 mwaka 2023 hadi 1,930 mwaka 2024, ikiwa ni upungufu wa asilimia 19.

Wizara imesema itaendelea kuimarisha mikakati ya uhamasishaji, elimu kwa jamii na mashirikiano na wadau mbalimbali ili kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua au kukomeshwa  kabisa katika jamii.