‘Wanaume kuleni tangawizi inaimarisha nguvu za kiume’

By Ashton Balaigwa , Nipashe
Published at 04:31 PM Jun 30 2025
Tangawizi
Picha:Mtandao
Tangawizi

BARAZA la Tiba Asili na Tiba Mbadala (TAHPC) Tanzania, limewataka wanaume nchini kujenga tabia ya kunywa chai ya tangawizi mara kwa mara, kwakuwa itawasaidia kuimarisha nguvu za kiume pamoja na mfumo wa uzazi.

Mwenyekiti wa baraza hilo la TAHPC, Prof. Joseph Otieno, amesema hayo wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro, kuhusu dhana ya tiba ya asili, tiba mbadala na sheria zake, kwa ajili ya kuendeleza na kumlinda mlaji.

“Wanaume wenzangu tujenge tabia ya kunywa chai ya tangawizi hata mara moja kwa siku ,inasaidia sana kwenye mfumo wa uzazi, kwa sisi kina baba kama ulikuwa unalima kidogo basi ukinywa, mambo yako yatakuwa mazuri utakuwa unalima shamba kubwa sana bila kuchoka” amesema Mwenyekiti huyo wa Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala.

Prof. Otieno, amesema pamoja na faida hiyo lakini faida nyingine ya kinywaji hicho cha tangawizi ni kuwa kinakunfanya usizeeke pamoja na kuwa na mzunguko wa damu mzuri katika mwili.