Wanawake katika siasa, bado mfupa mgumu

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 02:42 PM Mar 11 2025
Wanawake katika siasa, bado mfupa mgumu
Mchoro: Grace Mwakalinga
Wanawake katika siasa, bado mfupa mgumu

SIKU ya Wanawake Duniani, iliyoadhimishwa Machi 8, 2025 kitaifa jijini Arusha, Nipashe Digital imeandaa takwimu zinazoonesha ushiriki wa wanawake katika nafasi ya ubunge kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 katika siasa, bado mfupa mgumu

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura.

Kwa mujibu wa BBC, chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadae.

Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina Clara Zetkin.

Alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.

Kulikuwa na wanawake 100 hapo kutoka nchi 17 na wakakubaliana kwa pamoja.

Kwa mara ya kwanza ilisheherekewa mwaka 1911, Austria, Denmark,Ujerumani na Switzerland.

Sherehe ya 100 ilifanyika mwaka 2011, hivyo mwaka huu ni sherehe ya 107 ya wanawake duniani.