Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, amesema Prof. Philemon Sarungi alikuwa miongoni mwa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika kumaliza mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Amesema mgomo huo, ambao ulisababisha chuo kufungwa kwa muda, ulihitaji uchunguzi wa kina na mapendekezo madhubuti ili kutafuta suluhisho.
Kwa mujibu wa Warioba, Prof. Sarungi alipewa jukumu hilo na alitoa mapendekezo yaliyosaidia kumaliza mgogoro huo kwa mafanikio.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED