Wasira apokewa kwa kishindo Shinyanga

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 05:28 PM Mar 26 2025
Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira mkoani Shinyanga kwa ziara ya kuimarisha Chama.
Picha: Marco Maduhu
Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira mkoani Shinyanga kwa ziara ya kuimarisha Chama.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara Stephen Wasira,amepokelewa kwa kishindo mkoani Shinyanga.

Mapokezi hayo yamefanyika leo Machi 26,2025,wakati alipowasili mkoani humo kwa ajili ya shughuli za kichama. 

Wasira akizungumza wakati wa mapokezi hayo,amewashukuru wana CCM mkoani Shinyanga kwa mapenzi makubwa ambayo wameonyesha kwake, na kwamba ziara yake hiyo kuimarisha Chama. 

"Nawashukuru sana Wana CCM Shinyanga kwa mapokezi mazuri safari yangu hii Shabaha yake kubwa ni kuimarisha Chama. Chama chetu ni Chama kikubwa wala siyo cha Msimu kama vingine, baada ya uchaguzi vinakufa,na shughuli yetu sisi CCM ni kubadilisha maisha ya watu na kushughulikia matatizo yao ndiyo shabaha yetu ya msingi,"ameongeza.

 Aidha,amesema Chama hicho kimejinga vyema kwenye uchaguzi Mkuu mwaka huu, na kusema kwamba yajayo yanafurahisha. 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa,amemkaribisha Wasira mkoani humo na kwamba wanafura juu ya ugeni wake.

 Stephen Wasira ameanza ziara yake leo Machi 26 mkoani Shinyanga,na atahitimisha Machi 28,2025.